Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umewahikishia wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kupata makazi bora yanayokidhi mahitaji ya teknolojia ya kisasa.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya nyumba za makazi katika Maeneo ya Temeke Kota, Magomeni Kota na Masaki Mkurugenzi wa Idara ya Miliki FRV. Said Mndeme amesema TBA imeazimia kutekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ili kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba bora za makazi nchini.
Aidha, amesema anaishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kutenga fedha zaidi bilioni 60 ndani ya miaka miwili kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya za makazi.
“Katika eneo la Temeke Kota unaendelea ujenzi wa jengo moja la sakafu tisa (9) lenye uwezo wa kuchukua familia 144 ambapo mpango wetu kama Wakala ni kuhakikisha eneo hilo limakuwa na majengo saba yenye uwezo wa kuchukua familia 1008” amesema Mndeme.
Pia ametoa ufafanuzi juu ya miradi