Home KITAIFA TMDA INAVYOPIGA HATUA MADHUBUTI KIMATAIFA

TMDA INAVYOPIGA HATUA MADHUBUTI KIMATAIFA

Google search engine

*MAABARA YAKE SASA YATAMBULIWA WHO, NCHI ZA AFRIKA ZAJA KUJIFUNZA MAFANIKIO YAKE

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo akizungumza wakati wa Kikao kazi cha Wahariri na Waandishi wa habari kilichofanyika jijini Dar es Salaam
Kaimu Meneja Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Martha Malle, akitoa mada katika kikao kazi hicho kuhusu Sheria na Kanuni mbalimbali za udhibiti, za Mamlaka hiyo.

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), ni moja ya taasisi inayopata mafanikio nchini hasa baada ya nyota yake kung’ara huku maabara yake ya uchunguzi ikitambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Hatua hiyo ni mkakati wa TMDA wa kuhakikisha jamii inalindwa afya zao na inakuwa salama kutokana matumizi ya dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa nyinginezo zinazohusiana na afya.

Akizungumzia miaka 20 ya kuanzishwa kwa TMDA, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo amesema kuwa katika kipindi cha miongo miwili katika usimamizi wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kusimamia na kufanya uchunguzi katika eneo hilo kama njia ya kuhakikisha dawa na vifaa vyombo vinavyotumika vinakuwa na ubora unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.

“Jambo kubwa ambalo sisi kama mamlaka tunalosimamia ni kuhakikisha jamii ya Watanzania wanalindwa kwa kuwa na vifaa tiba pamoja na kuwa na matumizi sahihi ya dawa,” amesema Fimbo

Akieleza mafanikio yaliyopatika kwa mwaka 2011 maabara ya TMDA imetambuliwa kuwa mahiri ambapo ilimbuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO Prequlified Laboratory), 2012 kuwa Kituo cha umahiri wa usajili dawa barani Afrika na 2013 kuwa maabara ya mafunzo ya umahiri kwa Mamlaka za Udhibiti Dawa barani Afrika.

Fimbo, ameyataja mafanikio mengine kuwa ambapo mwaka 2014 walianzisha mifumo ya kielekroniki ya utoaji huduma Kwa wateja, 2015 Kutoa huduma za udhibiti kwa njia ya kielektroniki na kuimarika kwa makusanyo hivyo kuchangia asilimia 15ya mapato yake katika gawio la Serikali na kuwa na ziada ya asilimia 70.

“Mwaka 2017 tumefanikiwa kuanzisha mazingira wezeshi na rafiki ya ufanyaji biashara nchini kwa bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA, 2018 Kufikia Ngazi ya tatu ya Shirika la Afya Duniani – WHO (WHO Maturity L-3) kwa kuwa na mifumo bora ya udhibiti dawa barani Afrika.

“… hivyo kuwa taasisi ya kwanza ya udhibiti na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia ngazi hiyo na kupata hadhi ya juu ya ngazi ya nne umahiri wa Shirika la Afya Duniani (Quality Control LAB WHO ML 4),” amesema Fimbo

Pia kuzindua na kuanzisha Ofisi ya Kanda ya Ziwa, jijini Mwanza (sasa Kanda ya Ziwa Mashariki), kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa – TFDA (sasa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu TMDA na Kanda ya Mashariki)

Fimbo, ameyataja mafanikio mengine ni kuzindua rasmi jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa – TFDA (sasa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu TMDA na Kanda ya Mashariki), kuanzisha, kukidhi na kutekeleza mifumo ya utendaji kazi ya kimataifa ya ISO 1901:2018

Pia kupata tuzo ya kuwa taasisi ya kwanza yenye mifumo bora ya utendaji kazi Serikalini (Best Managed Institution in Tanzania), Maabara ya TMDA kuwa na umahiri unaotambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO Prequlified Laboratory) na Kituo cha umahiri wa usajili dawa barani Afrika.

MAABARA YA MAFUNZO

Mkurugenzi Mkuu huyo wa TMDA, amesema kuwa uwepo wa maabara ya mafunzo ya umahiri kwa Mamlaka za Udhibiti Dawa barani Afrika, kuanzisha mifumo ya kielekroniki ya utoaji huduma kwa wateja,Kutoa huduma za udhibiti kwa njia ya kielektroniki (automation of regulatory services)

Fimbo amesema kuwa hatua ya kuimarika kwa makusanyo hivyo kuchangia asilimia 15 ya mapato yake katika gawio la Serikali na kuwa na ziada ya asilimia 70 kama inavyoekekezwa na Hazina

Licha ya hilo pia kukamilisha ujenzi wa jengo la Ofisi ya TMDA Kanda ya Ziwa Mashariki Mwanza na kuanza kutumi, Kuanzisha mazingira wezeshi na rafiki ya ufanyaji biashar nchini kwa bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA

Pia Kufikia Ngazi ya tatu ya Shirika la Afya Duniani- WHO (WHO Maturity L-3) kwa kuwa na mifumo bora ya udhibiti dawa barani Afrika hivyo kuwa taasisi ya kwanza ya udhibiti na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia ngazi hiyo

Aidha amesema kuwa maabara ya TMDA kupata hadhi ya juu ya ngazi ya nne umahiri wa Shirika la Afya D\uniani, Kubadili jina kutoka TFDA kuwa TMDA, Kukamilisha ujenzi wa jengo la Ofisi ya TMDA Kanda ya Kati Dodoma na kuanza kutumika

Pia Mamlaka kupewa jukumu la udhibiti wa bidhaa za tumbaku,kuanzisha mfumo wa kufuatilia utoaji taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kwa njia ya simu

HATI SAFI YA CAG

Mafanikio mengine ni Mamlaka kupata hati safi kwa miaka 20 mfululizo kutokana na ukaguzi wa hesabu za taasisi kwa ukaguzi unaofanywa na ofisi ya CAG na kutimiza miaka 20 ya taasisi katika kulinda afya ya jamii kwa ufanisi.

Akifafanua pamoja na mafanikio tajwa, mamlaka inaendelea kuboresha huduma zake kwa kuzingatia maoni ya wateja. mathalan, kwa mujibu wa utafiti uuliofanywa na Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (University of Dar es Salaam Business School) wa Desemba 2020 kuhusu wateja kuridhika na huduma zitolewazo na Mamlaka.

Amesema katika halmashauri 28 kwenye mikoa 14 ya Tanzania, ulibaini kuwa asilimia 47 tu ya wananchi ndiyo wanaifahamu TMDA. Ni dhahiri kwamba matokeo haya yanaakisi mabadiliko ya jina la taasisi yaliyofanyika mwaka 2019.

“Hata hivyo, Mamlaka inatambua mchango wa vyombo vya habari katika kuongeza uelewa wa wananchi kuifahamu Mamlaka. Kwa kuwa upo umuhimu mkubwa wa wadau wote wa TMDA kuifahamu Mamlaka na majukumu yake.

“…Wahariri na Waandishi wa Habari wana wajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa Mamlaka inajulikana kwa jamii na Sheria tajwa inasimamiwa kiufanisi, TMDA imekuwa na utaratibu wa kukutana na wadau wake kwa lengo la kuwaelimisha juu ya kazi zake pamoja na majukumu ya kila mdau katika kutekeleza Sheria husika,” amesema

UELIMISHAJI JAMII

Kuhusu suala la uelimishaji jamii limepewa kipaumbele kikubwa na TMDA na ndiyo sababu tumewaita hapa Wahariri walioko mbele yako kwa lengo la kuwashirikisha mafanikio yaliyofikiwa na TMDA ili kujadiliana kwa pamoja namna ya kushirikiana zaidi katika kuhakikisha kuwa soko la Tanzania lina bidhaa zilizo bora, salama na fanisi ili kumlinda mlaji.

Fimbo, amesema kazi hii sio rahisi na inahitaji ushirikiano wa karibu kati yetu sisi TMDA, waandishi wa habari na wananchi wote kwa ujumla wao.

Amesema matumaini yao kupitia tasnia ya habari, wataweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwapa elimu endelevu ili waweze kufanya maamuzi sahihi wakati wa kuchagua, kununua na kutumia bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA kutoka katika soko.

“Ni imani yetu kuwa Wahariri na Waandishi hawa wakirudi kwenye maeneo yao ya kazi wataweza kueneza ujumbe watakaopata leo kwa watu wengi zaidi na hivyo kuwezesha jamii kupata elimu, kujilinda na kutumia dawa, vifaa tiba na vitendanishi vilivyosajiliwa au kupitishwa na TMDA,” amesema

MWANASHERIA WA TMDA

Akiwasilisha mada katika kikao kazi hicho, Kaimu Meneja wa Huduma za Sheria wa TMDA, Martha Malle, amesema kuwa Mamlaka ya Dawa Vifaa Tiba (TMDA) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya TMDA ilianzishwa chini ya Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba, Sura 219, huku lengo la kuanzishwa kwake ni  kudhibiti bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii.

Anasema TMDA iliundwa baada ya mabadiliko ya sheria yaliyofanyika kupitia Sheria ya Fedha Na. 8 ya mwaka 2019, ambapo udhibiti wa bidhaa za chakula na vipodozi ulihamishiwa TBS

Baada ya Mabadiliko haya ya kisheria, TMDA kwa sasa inathibiti bidhaa za dawa, vifaa tiba, vitendanishi na Tumbaku ambapo TMDA inasimamia

“Majukumu ya TMDA yameanishwa chini ya kifungu cha tano (5) cha Sheria ya TMDA, Sura 219 kama, kutathmini na kusajili dawa, vifaa tiba & vitendanishi, kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa kwa kudhibiti utengenezaji, uingizaji na usambazaji, kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kuhakikisha kuwa bidhaa husika zinafikia viwango vya ubora na usalama.

“Kusimamia majaribio ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi, kutoa leseni na vibali mbalimbali vya kuendeshea biashara ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi, kudhibiti uingizaji na utoaji nje ya nchi wa bidhaa, kudhibiti matangazo ya biashara ya bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA

“Kufuatilia madhara yatokanayo na matumizi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi, kuelimisha jamii kuhusu ubora, usalama na matumizi sahihi ya dawa, vifaa tiba & vitendanishi, kufanya ukaguzi wa bidhaa za dawa,vifaa tiba na vitendanishi kwenye soko,” amesema Malle

SHERIA YA WAKALA ZA SERIKALI

TMDA inafanya kazi kama Wakala wa Serikali  chini ya Sheria ya Wakala za Serikali, Sura 245 TMDA ni miongoni mwa Wakala 28 zilizopo hapa nchini.

“Lengo kubwa lililopelekea kuanzishwa wakala hizi za serikali lilikuwa ni  kuboresha na kusogeza huduma karibu na wananchi ili kuleta tija kwa Serikali. Kwa mujibu wa sheria, Wakala za serikali zinakuwa na Mkurugenzi Mkuu ambaye ndiye msimamizi Mkuu wa shughuli zote za Mamlaka

“Wakala za serikali zinakuwa na wajumbe wa Bodi ya Ushauri (MAB) ambao wanateuliwa na Waziri wa Afya. Majukumu ya Bodi ni kumshauri Waziri kuhusu utendaji kazi wa TMDA,”

KANUNI ZA UDHIBITI

Mwanasheria Malle, amesema kuwa TMDA ina jumla ya Kanuni 26 zinazosimamia maeneo yote ya udhibiti wa bidhaa zinazothibitiwa na mamlaka.

Amesmea kanuni hizo zimeainisha utaratibu na matakwa mbalimbali ambayo wafanyabiashara wanapaswa kuyafuata katika udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

“Kanuni hizi zinasaidia katika usimamizi wa sheria na kuweka utaratibu unaofanana wa kazi za udhibiti.Pia kuna miongozo mbalimbali iliyotengenezwa ili kumrahisishia mteja kupata uelewa mzuri kwa  huduma anayoihitaji TMDA,” amesema

ADHABU KWA MAKOSA MBALIMBALI

Mwanasheria Malle, amesema kuwa miongozo hii hutengenezwa kwa matakwa ya kanuni za mamlaka, ikiwamo bidhaa kwa ajili ya kusambazwa kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati za Serikali pia haziruhusiwi kusambazwa kwenye maduka ya watu binafsi.

“Kufanya uchakachuaji (adulteration) hakuruhusiwi, kufanya repacking and relabeling hakuruhusiwi pia kutoa matangazo bila kibali hakuruhusiwi vile vile bidhaa kwa ajili ya kusambazwa kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati za Serikali pia haziruhusiwi kusambazwa kwenye maduka ya watu binafsi

“Kwa mujibu wa Sheria Sura219, mtu yeyote anayekutwa na makosa tajwa hapo juu adhabu hutolewa, ikiwamo faini ya kati ya Shilingi 100,000 hadi milioni 10 au kifungo cha kati ya wiki mbili hadi miaka mitano au vyote kutegemeana na makosa,” amesema Malle

UTOAJI USHAHIDI MAHAKAMANI

Kitengo cha Sheria hushiriki kwenye mashauri yanayofikishwa Mahakamani, lengo ni kushirikiana na waendesha mashtaka ili kufafanua sheria na kusaidia katika kutoa ushahidi ili watuhumiwa waweze kuhukumiwa kwa makosa waliyoyafanya TMDA ina jumla ya kesi 27 zilizoko kwenye Mahakama mbalimbali hapa nchini.

“Majalada 62 yamefunguliwa kwenye vituo vya polisi ziko kwenye hatua za upelelezi, kesi zilizofungwa mahakamani pamoja na vituo vya polisi jumla ni 89 ikiwamo ushirikiano na Taasisi zingine katika kutekeleza Sheria.

“TMDA hushirikiana na taasisi kadhaa ikiwamo Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) pamoja na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Serikali(CPD).Drafters wa Sheria. Waendesha Mashtaka,  Mahakama,” amesema Mwanasheria Malle

Naye Meneja wa TMDA Kanda ya Mashariki, Adonis Bitegeko, amesema kuwa kazi za udhibiti katika soko na mipaka ambapo kazi za udhibiti za TMDA zinahusisha bidhaa za dawa (za binadamu, mifugo na chanjo), vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa za tumbaku.

“Kazi hizi hufanywa na TMDA hasa kupitia ofisi zake nane za Kanda, kazi za udhibiti katika kanda ikiwamo kusajili majengo (waingizaji bidhaa nchini na watengenezaji), kutoa vibali vya kuingiza bidhaa nchini.

“Pia tunafanya kazi ya ukaguzi katika mipaka na masoko ukusanyaji wa ufuatiliaji wa taarifa za madhara yanayotokana na matumizi ya dawa, chanjo na vifaa tiba, kukusanya sampuli za dawa na kupima katika maabara hamishika, kuimarisha ushirikiano na TAMISEMI katika kazi na majukumu yanayosimiwa na TMDA hususan ukaguzi, kusimamia uondoaji na uteketezaji wa bidhaa zisizofaa kwa matumizi,” amesema Bitegeko

MAFANIKIO

Amesema TMDA utekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Mpango Mkakati na Mpango kazi, ambapo kupitia utekelezaji huo TMDA imeweka na kuimarisha mifumo yake ambayo yafuatayo ni baadhi ya mafanikio ya udhibiti katika soko na mipaka.

“Usajili wa majengo kwa mwaka 2021/22, tulipokea maombi 870 ya usajili wa maeneo ya biashara, ya ambapo maombi 838 (97%) yaliidhinishwa na kusajiliwa na kupewa vibali vya biashara. 

“Idadi ya maeneo yaliyosajiliwa katika kipindi hiki ni ongezeko la maeneo 209 (33%) ikilinganishwa na maeneo 629 yaliyosajiliwa mwaka uliopita. Tulipokea maombi 1,035 ya usajili wa maeneo ya biashara ya dawa na vifaa tiba ambapo maombi 911 sawa na 89% yaliidhinishwa na kusajiliwa.

“…maeneo yaliyosajiliwa ni ongezeko la maombi 73 ikilinganishwa na maeneo 838 yaliyosajiliwa mwaka uliopita wa fedha. Ongezeko hili limechangiwa na uelewa wa wadau kuhusiana na taratibu na Sheria za kuendesha biashara ili kukidhi vigezo vya usalama na ubora pamoja na kuimarika kwa shughuli za kiuchumi,” amesema Bitegeko

UKAGUZI WA MAENEO 2021/22

Amesema maeneo 13,690 ya biashara za dawa na vifaa tiba yalikaguliwa, ukilinganisha na maeneo 10,846 kwa mwaka 2020/21.

“Aidha, maeneo 11,004 (80%) yalikidhi vigezo ikilinganishwa maeneo 8,364 ya mwaka 2020/21.  Ongezeko hili limechangiwa na kuimarika kwa shughuli za ukaguzi katika soko kufuatia Mamlaka kuongeza idadi ya wakaguzi na vitendea kazi.

“TMDA ilikagua maeneo 13,876 ya biashara za dawa na vifaa tiba ambapo maeneo 11,582 sawa na asilimia 84% yalikidhi vigezo. Maeneo yaliyokaguliwa katika kipindi hiki ni ongezeko la maeneo 186 (1.4%) ikilinganishwa na maeneo 13,690 yaliyokaguliwa katika kipindi kama hiki mwaka uliopita.

“Vilevile maeneo yaliyokidhi vigezo ni ongezeko la maeneo 578 ikilinganishwa na maeneo 11,004 yaliyokidhi vigezo katika kipindi kama hiki mwaka uliopita.  Ongezeko hili limechangiwa na kuimarika kwa shughuli za ukaguzi katika soko kufuatia Mamlaka kuongeza idadi ya wakaguzi na vitendea kazi,” amesema Bitegeko

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here