Home KITAIFA TANZANIA, MSUMBIJI KUENDELEA KUIMARISHA, KUDUMISHA USHIRIKIANO

TANZANIA, MSUMBIJI KUENDELEA KUIMARISHA, KUDUMISHA USHIRIKIANO

Google search engine
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax ambaye pia Mwenyekiti kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 15, 2023 baada ya kufunga kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji, katika kikao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax, Mwenyekiti kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 15, 2023 baada ya kufunga kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji, katika kikao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini  na Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Pascoal Ronda na mkalimani wake.

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

TANZANIA na Msumbiji zimekubaliana kuendeleza na kudumisha ushirikiano katika Ulinzi na Usalama kwa maslahi kwa Masilahi ya raia wan chi hizo mbili.

Hayo yamesemwa leo Septemba 15, 2023 Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax, baada ya kufunga kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji,  ambapo amesema kuwa Tanzania iko tayari kufanya kazi kwa karibu na nchi hiyo ili kuimarisha zaidi ushirikiano wa ulinzi na usalama.

Amesema kuwa kwa pamoja, tunaweza kushinda changamoto tunazokabiliana nazo na kujenga mustakabali ulio salama na wenye mafanikio zaidi kwa mataifa hayo mawili kwa watu wake.

“Uhusiano wa nchi hizi umejengwa kihistoria tangu wakati wa mapambano ya ukombozi kwa sababu tulipigana pamoja, kushinda pamoja na tunapaswa kubaki na umoja huo,” amesema Dk. Tax

Akizungumza baada ya mkutano uliowakutanisha watendaji wa juu katika idara mbalimbali za masuala ya ulinzi na usalama kutoka nchi Tanzania na Msumbji, Waziri Dk. Tax amesema kuwa mkutano huo ni matunda ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoifanya Septemba 27-29, 2022 alipotembelea nchini  Msumbiji iliyoendesha majadiliano.

Amesema mkutano huu umetoa fursa nyingine ya kuendeleza kushirikiano hasa katika maeneo ya mashirikiano yaliyomo katika mkataba wa makubaliano.

Kuhusu changamoto za uasi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Pascoal Ronda amesema uhusiano wa nchi hizo umekuwa na manufaa ya kihistoria.

“Juni 15 mwaka huu ikiwa ni baada ya miaka mingi ya mazungumzo magumu, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji pamoja na kiongozi wa chama cha Renamo alifunga kambi ya mwisho ya kijeshi ya vikosi vya kukabili vuguvugu la kigaidi huko Vunduzi, Wilaya ya Gorongosa, Mkoa wa Sofala.

“Hatua hii ya kihistoria inaashiria mwisho wa mchakato wa upokonyaji silaha, uondoaji na urejeshaji Silaha, uliofanyika kutokana na juhudi za ndani na nje ya Msumbiji na jumuiya ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Hatua hiyo inatoa mwelekeo wa maridhiano na utulivu wa nchi huku tukiwa na changamoto kubwa ya kupambana na ugaidi katika Jimbo la Cabo Delgado, ambako ni mapambano ya bila kupumzika huku tukiendelea na ushirikiano wa pamoja na jirani na ndugu zetu Tanzania,” amesema

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here