Home KIMATAIFA Peru: Kasisi wa Pacopampa afukuliwa baada ya miaka 3,000

Peru: Kasisi wa Pacopampa afukuliwa baada ya miaka 3,000

Google search engine
Mifupa inaonyesha mwili ulizikwa katika hali isiyo ya kawaida

Kaburi ambalo limekuwepo tangu 3,000 iliyopita limefukuliwa wakati shughuli ya uchimbaji kaskazini mwa Peru, mamlaka inasema.

Mtu aliyezikwa katika kaburi hilo alipewa jina la Kuhani wa Pacopampa na wanaakiolojia ambalo ni jina la eneo la nyanda za juu ambako kaburi hilo lilipatikana.

Watafiti walichimba tabaka sita za majivu yaliyochanganywa na udongo mweusi ili kufikia mifupa yake, ambayo iliambatana na mihuri miwili na matoleo mengine matakatifu.

Walielezea kupatikana kwa mifupa na vitu vilivyomo kama jambo la muhimu.

Vikombe na vitu vingine vya sanaa vilipatikana karibu na mwili

“Upatikanaji huo ni muhimu sana kwa sababu yeye ni mmoja wa makasisi wa kwanza kuanza kudhibiti mahekalu katika Andes kaskazini mwa nchi,” Bw Seki aliambia shirika la habari la AFP.

Eneo la Pacopampa, lililoko mita 2,500 juu ya usawa wa bahari, ni linajumuisha majengo tisa ya minara yaliyojengwa kwa mawe ya kuchonga yanayong’aa.

Inakadiriwa kuwa yamedumu kuanzia miaka 700 hadi 600 hivi kabla ya Kristo.

Uchimbaji huo ni juhudi ya pamoja zinayohusisha wanaakiolojia kutoka Makumbusho ya Kitaifa ya Ethnology nchini Japani na Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Peru cha San Marcos.

CHANZO: BBC

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here