Home KITAIFA PROFESA KITILA AKABIDHIWA RASMI OFISI, AWEKA WAZI MIKAKATI YA UWEKEZAJI NCHINI

PROFESA KITILA AKABIDHIWA RASMI OFISI, AWEKA WAZI MIKAKATI YA UWEKEZAJI NCHINI

Google search engine
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo(kulia), akikabidhiwa nyaraka na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji, leo Julai 28, 2023 jijini Dar es Salaam
aziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, akizungumza mara baada ya kukabidhi rasmi majukumu yake, kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara

NA MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

Wiki chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kufanya mabadiliko mabadiliko ya Baraza la Mawazirin a kuamua kumteua Mbunge wa Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, sasa waziri mpya amekabidhiwa rasmi majukumu mapya na kuweka wazi mkakati wa uwekezaji nchini.

Pamoja na hilo Profesa Kitila, amesema kuwa hatua ya kuwepo kwa sheria nzuri nchini kumeifanya Tanzania kuwa kimbilio kwa wawekezaji jambo ambalo lina manufaa kwa Taifa na watu wake.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 28, 2023 wakati akizungumza mara baada ya kukabiwa ofisi na Waziri wa Viwand ana Biashara, Dk. Ashatu Kijaji ambapo pamoja na mambo mengine alikabidhiwa majukumu hayo ikiwa ni ishara ya kuanza majumu.

Makabidhino hayo yamefanyika katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Jijini Dar es Salaam,  ambapo amesema kuwa amepokea masuala manne ambayo ataendelea kuyatekeleza kwa kasi ili kuwezesha wawekezaji kuvutiwa kuja kuwekeza nchini.

“Kufuatia auamzi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, wa kuunda Wizara mpya ya Mipango na Uwekezaji, leo Waziri wa Viwanda na Biashara amenikabidhi kipande cha Uwekezaji ambacho kilikuwa chake na amenikabidhi mambo manne ikiwemo mchakato wa mabadiliko ya Sera ya Uwekezaji ya mwaka 1996, amenikabidhi Sheria Mpya ya Uwekezaji na Kanuni zake ya mwaka 2022 ambayo ilipitishwa Bungeni hivi karibuni,” amesema Prof. Kitila

Amesema katika makabidhiano hayo pia amekabidhiwa bajeti ya mwaka 2023/24 kwenye kipande cha uwekezaji akibainisha kuwa jukumu la wizara hiyo ni kuvutia wawekezaji ili kukuza uchumi wa nchi

Profesa Kitila amesema kuwa wizara hiyo ina jukumu kubwa ambalo ni kuendelea kuvutia wawekezaji wakubwa kutoka sehemu mbalimbali duniani na kutoka ndani ya nchi, huku akitaja  utulivu na utashi wa kisiasa pamoja na  mazingira mazuri ya kisheria ni mambo ambayo yanavuta wawekezaji wengi kutoka nje ya nchi.

Kwa Upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji amesema kuwa tangu apatiwe kipande cha uwekezaji hapo Januanri 2022 wameweza kusajili miradi 522 katika sekta mbalimbali hapa nchini.

“Kwa mwaka uliopita tangu nimeaminia na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na kupewa kipande hiki cha uwekezaji tumesajili miradi 522 kuanzia januari 2022 mpaka sasa hapa ninapokukabidhi sekta hii ambayo ni muhimu kwa nchi,” amesema Dk Kijaji

Amesema kuwa usajili wa miradi hiyo utawezesha upatikanaji wa ajira 72,000 na kupunguza changamoto ya ajira nchini lakini pia katika uwekezaji huo nchi itapata mapato na kuinua uchumi wa Watanzania.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here