Home KITAIFA TANESCO YATAMBA KUVUNJA REKODI YA MAPATO YAKE, KUONGEZA IDADI YA WATEJA

TANESCO YATAMBA KUVUNJA REKODI YA MAPATO YAKE, KUONGEZA IDADI YA WATEJA

Google search engine
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande akieleza mikakati ya shirika hilo mbele ya wahariri wa habari jijini Dar es Salaam leo, Julai 27, 2023
Mkurugenzi wa Huduma za Wateja wa Tanesco, Martine Mwambene, akitoa ufafanuzi wa shughuli za kurugenzi yake kwa wahariri wa vyombo vya habari
Baadhi ya wahariri waliohudhuria kikao kazi cha Shirika la Umeme Tanzania

NA MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limetamba kuvunja rekodi ya mapato kwa mwaka 2021/22 na kufikia faida ya Sh Trilioni 1.8 ikiwa ni tofauti na mwaka wa fedha uliopita ambayo ni sawa na asilimia 11.

Katika mwaka wa fedha uliopita Tanesco ilipata faida ya Sh Trilioni 1.6 ya mauzo yake.

Akizungumza leo Julai 27, 2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha Tanesco, Renatha Ndege, katika mkutano ulioandaliwa chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wahariri wa Vyombo vya Habari, ambapo amesema kuwa hayo ni mafanikio makubwa kwa shirika hilo ambalo kwao wanaona ni fahari kuona wanazidi kusonga mbele hasa kutokana na usimamizi Madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Kutokana na kuwa na mikakati kadhaa Madhubuti ndani ya Tanesco, Ndege amesema kuwa kwa sasa hawatengenezi hasara bali ufanisi umekuwa uikiongezeka kila mwaka kwa kupata faida lukuki.

“Hali ya fedha inaendelea kuboreka mwaka hadi mwaka, mwaka jana tumepata faida Sh bilioni 109.4 kutoka Sh bilioni 77 za mwaka 2021 ongezeko aslimia 42 na pia tumeongeza uzalishaji Pamoja na watenja maboa kwa mwaka wa fedha uliopita tumepata wateja Zaidi ya 500,000.

Awali akizungumza katika kikao kazi hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Maharage Chande, amesema utekelezaji wa mradi wa uzalishaji umeme katika Bwawa la Julius Nyerere umefikia asilimia 90 na kwamba Juni 2024 watawasha umeme.

“Mradi huu ni muhimu kwa sababu unagharimu Dola zaidi ya bilioni 3.5 na umeme huu ukipatikana utatosheleza mahitaji hata zikiungwa nyumba zote Tanzania,” amesema Chande.

Mkurugenzi huyo wa Tanesco, alieleza mkakati wa shirika hilo, ikiwamo kuanzisha utaratibu wakuajiri wafanyakazi waliokuwa wa vibarua na mikataba kwa kuwajumuisha katika ajira za kudumu ikiwa ni mkakati wa kuimarisha rasilimali watu.

“Awali kulikuwa na malalamiko mengi ya wafanyakazi na kuthibitishwa kutokuwa na mikataba lakini hivi sasa wamelitatua hili na kuboresha muundo wa utumishi ndani ya shirika,”amesema Chande

Amesema kila mwaka wanachagua wafanyakazi 20 kutokana na utendaji wao kisha kuwapeleka kwenye mafunzo nje ya nchi ambapo huwaunganisha kwenye kampuni kubwa ili kuwaandaa kurithi nafasi mbalimbali ndani ya shirika hilo.

Amesema hivi sasa watumishi hao wapo  nchini Afrika Kusini na tayari wameingia makubaliano na nchi nyingine kama Algeria kupeleka wafanyakazi kupata ujuzi zaidi.

“Tumeandaa ‘Graduate trainee programme’ ambapo kila mwaka tutauwa tukichukua wanafunzi 50 wa vyuo vikuu kwa ajili ya kuwapa mafunzo zaidi. Kutokana na hizi program miaka mitatu baadaye tunaamini watu watakuwa na hamu ya kuja kufanya kazi Tanesco,” amesema Chande.

Aidha kwa mwaka 2021/22 shirika hilo lenye wateja milioni 4 limewaunganishia umeme wateja wapya 504,366.

Amesema kwa mwaka 2020/2021 gharama ya uzalishaji wa umeme ulikuwa Sh1.5 trilioni ikilinganishwa na ongezeko la Sh 1.6 trilioni kwa mwaka 2021/2022.

MRADI UMEME WA MWALIMU NYERERE

“Mradi wa Mwalimu Nyerere ukikamilika gharama za umeme zitashuka lakini hatutashusha bei kwasababu tutashindwa kwenda,”amesema.

Chande alitoa mchanganuo wa matumizi ya umeme kwamba mpaka sasa shirika hilo linawateja milioni 4.4, ambao miongoni mwao wateja wa viwandani ni 4,000 na majumbani zaidi ya milioni tatu.

Kiwango hicho kinawafanya wananchi kutumia asilimia 50 ya megawati 1400 zinazozalishwa na Tanesco kila siku na viwanda nako ni asilimia 50.

UPOTEVU WA UMEME

Kuhusu upotevu wa umeme, Makamu Mkurugenzi wa uzalishaji umeme Tanesco, Pakaya Mtamakaya amesema mwaka 2020/2021 upotevu ulikuwa wa asilimia tisa lakini kufikia 2021/2022 upotevu ukipungua kufikia asilimia 8.

Amesema sababu ya upotevu wa umeme ni umeme wenye kilovoti ndogo kusafirishwa umbali mrefu na sasa wanaendelea na mkakati wa kupunguza upotecy wa umeme.

Ifikapo Juni, 2024 mradi huo utaanza kuzalisha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amelipongeza shirika hilo kwa kazi kubwa inayofanya na kusema ni taasisi ya mfano wa kuigwa.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here