Home KITAIFA KINANA: RAIS DK.SAMIA ANAFANYA KAZI KUBWA, ATIWE MOYO

KINANA: RAIS DK.SAMIA ANAFANYA KAZI KUBWA, ATIWE MOYO

Google search engine
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, akihutubia mkutano wilayani Rufiji mkoani Pwani leo, wakati wa hafla ya kukabidhi vitendea kazi kwa watendaji wa Jimbo la Rufiji, vilivyonunuliwa na Mbunge wa jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema Rais Dk.Samia Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kuleta maendeleo kwa Watanzania katika kipindi kifupi cha uongozi.

Hivyo kinachopaswa kufanywa na kila mmoja ni kumuunga mkono, kumpa moyo na kuthamini yale anayofanya.

“Rais Samia ameongoza kwa miaka miwili, kama alivyosema Waziri wa Maliasili na Utali Mohamed Mchengerwa, haya ambayo mbunge anayasema yanafanyika katika kila jimbo nchini, kuna shughuli nyingi zinaendelea na Rais wetu si mtu wa kujitukuza, sio mtu wa kujisifia, yeye ni mtu wa vitendo

“Kila mahali katika nchi hii kuna kazi zinafanyika, miundombinu ya barabara, maji, hospitali, ujenzi wa shule na kwa mara ya kwanza wazazi hawajaambiwa wachange kujenga shule na kununua madawati, katika historia ya nchi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka miwili zaidi ya madarasa 20,000 yamejengwa,” alisema.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here