Home KITAIFA KAMATI YA TENDAJI MRADI WA KUPAMBANA NA UJANGILI, BIASHARA HARAMU YAKUTANA ARUSHA

KAMATI YA TENDAJI MRADI WA KUPAMBANA NA UJANGILI, BIASHARA HARAMU YAKUTANA ARUSHA

Google search engine

NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

NA MWANDISHI WETU 

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbasi leo Julai 10, 2023 akiwa na Mwenyekiti Mwenza ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Christine Musisi, ameongoza Kikao cha Kamati Tendaji ya Mradi wa Kupambana na Ujangili na Biashara Haramu ya Nyara. Mradi huu ni utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Ujangili na Biashara Haramu ya Nyara. 

Mradi huu umesaidia sana Serikali katika kukabiliana na ujangili na biashara  haramu ya wanyamapori hususani tembo kwa kuwezesha Doria,  ununuzi wa vifaa yakiwemo magari 10, kutoa mafunzo,  kuwezesha miradi kwa jamii na kuanzisha WMA ya Chamwino

Mradi huo unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Kimataifa “Global Environmental Facility” (GEF) na UNDP kwa jumla ya USD 6,354,587.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here