Home KITAIFA Hatima ya Balozi Karume mikononi mwa Rais Samia

Hatima ya Balozi Karume mikononi mwa Rais Samia

Google search engine

*Mwenyewe alitabiri mwanzo, mwisho wake CCM

Balozi Ali Karume

Na Mwandishi Wetu

-Zanzibar

HATIMA ya uanachama kwa kubariki kufukuzwa ama kusalia ndani ta Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kada wa chama hicho Balozi Ali Karume sasa imebaki mikononi mwa Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Hilo limekuja baada ya Halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja ikitangaza kutoa mapendekezo ya kumfuta uanachama kada wake Balozi Ali Karume, mwenyewe alitabiri mwisho wake.

Vikao vya ngazi ya juu ya CCM vinaanza leo Julai 8, 2023 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, kilichoketi jana Julai 7, 2023 chini ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Juni 18, 2023 Balozi Karume, alisema kuwa kadi ya CCM mara ya mwisho nilijaribu kuitumia kwenye ATM lakini haikufanya kazi hivyo kwake American Express na Viza ni muhimu kuliko kadi ya chama hicho tawala nchini.

Kwa mujibu taarifa iliyosambaa leo Julai 8, 2023 asubuhi ilielezwa kuwa kikao cha kupendekeza kumfuta uanachama Balozi Karume kimefanyika saa saba usiku wa kuamkia leo Jumamosi Julai 8, 2023 chini ya Katibu wa Mkoa wa CCM, Amina Mnacho.

Taarifa ya kumuondosha kwenye chama hicho ilitolewa na Katibu Mwenezi wa Mkoa huo, Ali Timamu Haji.

Hatua hiyo inakuja baada ya chama hicho kumpa onyo kutoka na kauli zake zake akidaiwa kukidhalilisha chama na kuwatukana viongozi wakuu hadharani.

Awali Juni mwaka huu, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Ali Abeid Karume alihojiwa Kamati ya Maadili ya chama hicho huku akiweka wazi kwamba yupo tayari kupokea uamuzi wowote dhidi yake.

Hatua ya kuitwa kwenye vikao vya maadili ya imekuja baada ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Zanzibar kuonya baadhi yaw ana CCM kuvunja maadili na utamaduni wa chama hicho kwa kuzusha mambo ambayo yanahatarisha uhai wa CCM na kuwapo kwa mgawanyiko.

Hivi karibuni hivi karibuni katika moja ya mijadala kwenye mitandao ya kijamii, alisema CCM kipo madarakani si kwa sababu kilishinda uchaguzi, bali kwa sababu ya uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Kada huyo pamoja na hali hilo pia alikosoa uamuzi wa Rais  wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi wa kukodisha visiwa vilivyopo Zanzibar kwa wawekezaji.

Kutokana na hali hiyo ambayo ilionekana kuzusha taharuki ndani ya chama hicho tawala ambapo Rais Mwinyi aliagiza wanachama wote wanaotoa kauli za kuwagawa na kukiyumbisha chama wasiachwe hadi nyakati za uchaguzi, bali wachukuliwa hatua mapema.

Kauli hizo zilimfanya Balozi Karume kuhojiwa na na chama hicho tawi la Mwera, Juni 15, 2023 na alihojiwa na Kamati ya Maadili ya jimbo la Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja na Juni 16, 2023 alihojiwa na Kamati ya Maadili Wilaya ya Kati, mkoani humo.

Akizungumzi hatua hiyo, Balozi Karume amesema kikao hicho kilidumu kwa saa moja, akidai nusu saa ilikuwa ya mazungumzo maalumu na nusu saa nyingine ilikuwa ya kutaniana na kuwapa hadithi.

Alipoulizwa atahamia chama gani iwapo atafukuzwa CCM, alijibu kuwa hajajiandaa kufukuzwa uanachama na ikitokea hawezi kuhamia chama kingine chochote cha siasa, kwa sababu moyo na mapenzi yake bado yapo ndani ya CCM.

Amesema katika vikao vyote alivyoitwa mazungumzo yalikuwa mazuri na zaidi yalilenga kuhoji masuala ya uchaguzi ndani ya CCM.

Kuhusu taarifa zilizosambaa mtandaoni zikionyesha amesema kadi yake ya American Express na Viza ni muhimu kuliko kadi ya CCM, Balozi Ali alisema, “Ndiyo nimesema kwa sababu kadi ya CCM mara ya mwisho nilijaribu kuitumia kwenye ATM lakini haikufanya kazi.” amesema

“Zanzibar kama unafanyika uchaguzi wa haki na wazi mgombea wa CCM hawezi kushinda kwa sababu wagombea huletwa kutoka CCM Taifa na hawafuati ushauri au kuzingatia matakwa ya wanachama wake, hili nililisema na ninaweza kulirejea tena.”

“Pia mtu akiulizia mchakato wa uchaguzi haina maana kwamba anapinga mgombea wa CCM kushindwa, nia yangu ni kujenga tujipange vizuri ili tushinde katika uchaguzi mkuu ujao,” amesema Balozi Karume

Hata hivyo kwa mujibu wa Katiba ya CCM inaelekeza kwamba Halmashauri Kuu ya CCM ndiyo chombo cha mwisho cha maamuzi mwisho dhidi ya hatua yoyote ya chama au mwana chama.

Kutokana na hali hiyo ambapo sasa ikiwa maamuzi hayo yatafikishwa mbele ya vikao hivyo vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ambavyo Mwenyekiti wake ni Rais Dk. Samia Suluhu Hassan nayo inatarajiwa kukutana na kusaidiwa na makamu wake Dk. Hussein Ali Mwinyi na Abdulrahman Kinana.

Taarifa iliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi, inaeleza kwamba vikao vya Kamati Kuu ya chama hicho (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) chini ya Mwenyekiwa wake Rais Dk. Samia Suluhu Hassan vitaanza kuketi kesho Julai 9, 2013 Jijini Dodoma.

“Vikao hivyo vya kawaida vya uongozi wa chama ngazi ya Taifa, vitafanyika kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya Mwaka 1977, Toleo la 2023, vikitanguliwa na kikoa cha Sekreterietyi ya Halmashauri Kuu ya CCM itakayoketi Julai 8 (leo) 2023,” ilieleza taarifa ya CCM iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Sophia Mjema.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here