Home KITAIFA JK AMPONGEZA RAIS SAMIA MAANDALIZI UZINDUZI PROGRAMU YA UWEKEZAJI SEKTA YA MAJI...

JK AMPONGEZA RAIS SAMIA MAANDALIZI UZINDUZI PROGRAMU YA UWEKEZAJI SEKTA YA MAJI TANZANIA 2024-2030

Google search engine
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Water Partnership Southern Africa (GWPSA), kulia ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na kushoto ni Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi

Na Mwandishi Wetu

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Water Partnership Southern Africa (GWPSA) na Mwenyekiti Mwenza Mbadala (Alternative Co-Chair) wa Continental Africa Water Investment Programme High-Level Panel amempongeza Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kwa kukamilisha na kuanza maandalizi ya uzinduzi wa Program ya Uwekezaji Katika Sekta ya Maji Tanzania.

Akizungumza na viongozi na watumishi wa Wizara ya Maji, Kikwete ameelezea furaha yake kwa Tanzania kupitia Wizara ya Maji kuandaa Programu ya Uwekezaji katika Sekta ya Maji Tanzania (Tanzania Water Investment Programme) katika kipindi cha mwaka 2024-2030.
Programu hiyo inayokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 15 inahusisha Sekta za Maji, Nishati, Mazingira, Afya, Uvuvi, Kilimo, Madini, Mifugo, Utalii, Mali Asili na Viwanda miongoni mwa Sekta nyingine.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumzia swala hili amesema Madhumuni ya Programu hiyo ni kuhakikisha kuwa Taifa linakuwa na usalama wa maji na uwezo wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame na mafuriko ili kuwezesha upatikanaji wa maji ya kutosha na yenye ubora kwa ajili ya matumizi ya watu, shughuli za uchumi na mazingira.

Programu hiyo yenye maeneo manne ya maji na jamii, maji na uchumizi; maji na mabadiliko ya tabianchi na usimamizi na uongozi katika maji itaongeza msukumo katika ujenzi wa miradi mikubwa ya maji yakiwemo mabwawa kwa ajili ya mifugo na kilimo miongoni mwa matumizi mengine.

Programu hiyo ambayo ni agenda ya Umoja wa Afrika ina wadau mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa wakiwemo Mashirika ya UNDP, UNICEF, GWP na Global Centre for Adaptation na inaratibiwa na Taasisi ya GWPSA.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here