Home KITAIFA Balozi Karume: Nipo tayari kupokea uamuzi wowote CCM

Balozi Karume: Nipo tayari kupokea uamuzi wowote CCM

Google search engine

Ni baada ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili CCM, hatima yake yabaki kwa Rais Samia, Dk. Mwinyi

Balozi Ali Abeid Aman Karume

Na Mwandishi Wetu

-Zanzibar

Mtoto wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Ali Abeid Karume amehojiwa na Kamati ya Maadili ya chama hicho huku akiweka wazi kwamba yupo tayari kupokea uamuzi wowote dhidi yake.

Hatua ya kuitwa kwenye vikao vya maadili ya imekuja baada ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Zanzibar kuonya baadhi yaw ana CCM kuvunja maadili na utamaduni wa chama hicho kwa kuzusha mambo ambayo yanahatarisha uhai wa CCM na kuwapo kwa mgawanyiko.

Hivi karibuni hivi karibuni katika moja ya mijadala kwenye mitandao ya kijamii, alisema CCM kipo madarakani si kwa sababu kilishinda uchaguzi, bali kwa sababu ya uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Kada huyo pamoja na hali hilo pia alikosoa uamuzi wa Rais  wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi wa kukodisha visiwa vilivyopo Zanzibar kwa wawekezaji.

Kutokana na hali hiyo ambayo ilionekana kuzusha taharuki ndani ya chama hicho tawala ambapo Rais Mwinyi aliagiza wanachama wote wanaotoa kauli za kuwagawa na kukiyumbisha chama wasiachwe hadi nyakati za uchaguzi, bali wachukuliwa hatua mapema.

Kauli hizo zilimfanya Balozi Karume kuhojiwa na na chama hicho tawi la Mwera, Juni 15, 2023 na alihojiwa na Kamati ya Maadili ya jimbo la Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja na Juni 16, 2023 alihojiwa na Kamati ya Maadili Wilaya ya Kati, mkoani humo.

Akizungumzi hatua hiyo, Balozi Karume amesema kikao hicho kilidumu kwa saa moja, akidai nusu saa ilikuwa ya mazungumzo maalumu na nusu saa nyingine ilikuwa ya kutaniana na kuwapa hadithi.

Alipoulizwa atahamia chama gani iwapo atafukuzwa CCM, alijibu kuwa hajajiandaa kufukuzwa uanachama na ikitokea hawezi kuhamia chama kingine chochote cha siasa, kwa sababu moyo na mapenzi yake bado yapo ndani ya CCM.

Amesema katika vikao vyote alivyoitwa mazungumzo yalikuwa mazuri na zaidi yalilenga kuhoji masuala ya uchaguzi ndani ya CCM.

Kuhusu taarifa zilizosambaa mtandaoni zikionyesha amesema kadi yake ya American Express na Viza+ ni muhimu kuliko kadi ya CCM, Balozi Ali alisema, “Ndiyo nimesema kwa sababu kadi ya CCM mara ya mwisho nilijaribu kuitumia kwenye ATM lakini haikufanya kazi.” amesema

“Zanzibar kama unafanyika uchaguzi wa haki na wazi mgombea wa CCM hawezi kushinda kwa sababu wagombea huletwa kutoka CCM Taifa na hawafuati ushauri au kuzingatia matakwa ya wanachama wake, hili nililisema na ninaweza kulirejea tena.”

“Pia mtu akiulizia mchakato wa uchaguzi haina maana kwamba anapinga mgombea wa CCM kushindwa, nia yangu ni kujenga tujipange vizuri ili tushinde katika uchaguzi mkuu ujao,” amesema Balozi Karume

Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Kati, Omar Moric amesema kada huyo aliitikia wito na alifika kwa wakati katika vikao vyote viwili, cha jimbo na wilaya, akiwa amevaa sare za chama, lakini hakuwa tayari kueleza yaliyojadiliwa.

Hata hivyo kwa mujibu wa Katiba ya CCM inaelekeza kwamba Halmashauri Kuu ya CCM ndiyo chombo cha mwisho cha maamuzi mwisho dhidi ya hatua yoyote ya chama au mwana chama.

Kutokana na hali hiyo ambapo sasa ikiwa maamuzi hayo yatafikishwa mbele ya vikao hivyo vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ambavyo Mwenyekiti wake ni Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na kusaidiwa na makamu wake Dk. Hussein Ali Mwinyi na Abdulrahman Kinana.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here