Home KITAIFA CHONGOLO AONGOZA HARAMBEE YA KUCHANGIA NYUMBA YA BALOZI SHINA NO 7 –...

CHONGOLO AONGOZA HARAMBEE YA KUCHANGIA NYUMBA YA BALOZI SHINA NO 7 – KISING’A -IRINGA

Google search engine
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo, akizungumza na wanachama wa CCM wakati wa harambee hiyo

Na Mwandishi Wetu

-Iringa

Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo leo tarehe 30 Mei 2023 amepokelewa na wananchi pamoja na wanachama wa CCM kata ya Kising’a Jimbo la Isimani Shina No 7 kwa Balozi Rose John

Pamoja na mambo mengine Ndg Chongolo ameongoza Harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya balozi Rose John kutoka nyumba ya kupanga na kupata nyumba yake ya kuishi ya kisasa na yenye hadhi ya Balozi wa CCM Shina No 7 kata ya Kising’a.

Ndg. Chongolo ameongozana na wajumbe wawili wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Issa Gavu – Katibu wa Idara ya Organaizesheni na Sophia Mjema – Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, huu ni mwendelezo wa ziara ya katibu Mkuu wa CCM ya kuimarisha Chama katika Ngazi zote na kutatua Changamoto za wananchi Mkoa wa Iringa.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here