Home KIMATAIFA Rais Museveni apitisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja Uganda

Rais Museveni apitisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja Uganda

Google search engine

NA MWANDISHI

Spika wa Bunge la Uganda ametangaza kuwa Rais Museveni ameutia saini muswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja kuwa sheria.

Spika Anita Among, amesema Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, ametekeleza majukumu yake ya kikatiba kama ilivyoainishwa na Ibara ya 91 (3) (a) ya Katiba. Ameidhinisha Sheria ya Kupinga mapenzi ya jinsia moja, aliandika katika taarifa yake aliyoituma kwenye mtandao wa Twitter.

”Kama Bunge la Uganda, tumejibu kilio cha wananchi wetu. Tumetunga sheria ili kulinda utakatifu wa familia kulingana na Kifungu cha 31 cha Katiba ya Uganda”.

”Tumesimama kidete kutetea utamaduni wetu na matarajio ya watu wetu kulingana na malengo ya 19 & 24 ya malengo ya kitaifa na kanuni za maagizo ya sera ya serikali. Namshukuru Mheshimiwa Rais, kwa hatua yake thabiti kwa maslahi ya Uganda.”, aliandika Spika Anita Among.

Aliongeza kuwa ”Kwa Mungu na Nchi yangu, Daima tutasimamia na kuendeleza maslahi ya watu wa Uganda”

Aliwashukuru wananchi wa Uganda kwa ”maombi na kutia moyo tulipotekeleza wajibu wetu” kwa mujibu wa Ibara ya 1 na 79 ya Katiba.

Amewataka watekelezaji kutekeleza mamlaka waliyopewa kisheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja.

Ikulu ya Uganda katika ukurasa wake wa Twitter imetuma picha ya Museveni kuthibitisha kuwa rais huyo ametia saini muswada:

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here