Home KITAIFA Chongolo: CCM inahitaji Katiba bora kuliko mtu

Chongolo: CCM inahitaji Katiba bora kuliko mtu

Google search engine
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, akizungumza na wananchi wilayani Mufindi

Na Mwandishi Wetu

-Iringa

Katibu Mkuu wa Cha Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema chama hicho kinahitaji katiba bora kuliko mtu yeyote.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa tayari chama hicho tawala kimetoa ridhaa kwa Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumapili Mei 28, 2023 katika ziara yake inayoendelea wilayani Mufindi Mkoani Iringa, ambapo  Chongolo ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Idara ya Oganizesheni, Issa Haji Ussi, ambapo amesema kuwa hata rasimu ya Katiba iliyokuwa imeandaliwa miaka tisa iliyopita, imepitwa na muda.

“Chama cha Mapinduzi kimempa ridhaa na dhamana Mwenyekiti (Rais Samia Suluhu Hassan) kuanzisha mchakato wa mapitio kuangalia iwe namna gani na iandikwaje? Ndiyo kazi tunafanya. Hamjamsikia Mwenyekiti wa CCM akitamka?” alihoji Chongolo na kuongeza;

“Hamjasikia akisema sasa naangalia mazingira ya kuanzisha mchakato tuone, na tuchukue katiba ipi twende nayo? Tuna katiba ya mwaka 1977 imetufikisha leo hapa tuna amani, utulivu na nchi inaenda, kweli si kweli?,” amesema na kuhoji Chongolo.

Mtendaji Mkuu huyo wa CCM alikuwa akisalimiana na wananchi wa mji wa Mafinga, Wilayani Mufindi waliofika kumlaki wakati alipowasili Mkoani Iringa jana Mei 26, 2023 kwa lengo la kuanza ziara ya kikazi pamoja na kukagua uhai wa chama.

Aidha amekumbusha kuwa lipo andiko la katiba inayo pendekezwa ambalo halijafika mwisho na sasa ni zaidi ya miaka tisa tangu liandikwe.

“Tunarudi na kitabu cha miaka tisa? Tuna mambo yanatakiwa kupitiwa tuyaweke yaendane na wakati wa sasa, ukienda Saohill kuchukua kitabu cha kuvuna ni sawa na leo? Dunia imebadilika na mambo yameenda spidi, tunataka tuendane na mazingira ya sasa,” amesisitiza Katibu Mkuu huyo wa CCM.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here