Home KITAIFA Uharibifu wa mazingira unavyoathiri baonuai nchini

Uharibifu wa mazingira unavyoathiri baonuai nchini

Google search engine
Meneja Ufuatiliaji na Tathmini, RTI, Mshirika mtekelezaji wa USAID inayotekeleza Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, John Noronha (katikati) akiwasilisha mada katika mjadala wa asubuhi wa Wahariri uliondaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET).Kulia ni Mkuu wa Sehemu Utangazaji Utalii Ikolojia, Anna Lauwo na kushoto ni mwendesha mjadala huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa JET, Dk. Ellen Ottaru

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

JAMII imetakiwa kutambua kwamba suala la uharibu wa mazingira imekuwa ni kichocheo cha upotea Baonuai nchini.

Kutokana na hali hiyo waandishi wa habari nchini wametakiwa kuelisha jamii kuhusu suala la utunzani wa mazingira kama njia ya kulinda shoroba na baonuai kwa viumbe vya majini na kwenye maeneo ya hifadhi kwani hatua hiyo itasaidia kuona mchango wa kwenye pato la Taifa

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa ulioratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kupiitia mradi wa unaotekelezwa na USAID wa Tuhifadhi.

Dk. Elikana Kalumanga ambaye ni Meneja Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi, RTI, Mshirika mtekelezaji wa USAID inayotekeleza Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, akiwasilisha mada

Akizungumza katika mkutano huo, Meneja Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi RTI, mshirika mtelekezaji wa USAID inayotekeleza Mradi wa USAID Tuhifadhi, Dk. Elikana Kalumanga baonuai ni pamoja na aina milioni nane za mimea na wanyama wanaopatikana kwenye sayari, mifumo ya ikolojia inayotumika kama makazi yake pamoja na utofauti wa kimaumbile.

“Hili jambo ni mtambuka na ni lazima sisi kama wana jamii tukiri kwamba bado jamii yetu haina uelezwa wa kutosha kuhusu muhimu wa baoanuai licha ya ukweli kuwa ndivyo vitu vinavyotuzunguka katika maisha yetu ya kila siku na kufanya dunia kuwa mahala salama pa kuishi nyakati zote.

“Kwa mfano kuna vitu kama bahari, maziwa, mito, mabonde pamoja na msitu ambao ndio ni moja ya kutengeza baonuai. Kwa mfano hapa Dar es Salaam tunafurahia kuona tunapata hewa nzuri na maji ya kunywa bila kuzingatia kuwa kuna sehemu yanatoka. Hapa niseme tu kwamba mapafu ya Dar es Salaam ni msitu wa Kazimzumbwi kama tukiuharibu ni wazi tutakuwa na hali mbaya hivyo ni vema jamii ikubali kuona tuna wajibu wa kulinda misitu yetu ili kulinda baonuai

“Ukija katika eneo la misitu miti kama miyombo hasa katika mikoa ya Tabora, Kagera…mikoko na aina nyingine ambayo hii inachochea sana uwepo wa baoanuai lakini kutokana na jamii yetu kutokuwa na ufahamu wa kutosha imekuwa ikiikatwa ovyo bila kujua athari zake kwa jamii,” amesema Dk. Kalumanga.

Kutokana na hali hiyo Dk. Kalumanga amesema kuwa hadi sasa kama nchi bado hatujapata mchango halisi na hata kufanya tathimini ya kina wa baoanuai katika pato la taifa.

“Ni wajibu kwa wana habari kuona kwamba mna kazi kubwa ya kuendelea kutoa elimu kwa jamii, mtu ajue kwamba kumbe misitu mbali na kupata mbao tu kuna faida nyingine inayopatikana, au maji siyo kutupa samaki tu kumbe kuna faida nyingine,” amesema.

Naye Meneja Ufuatiliaji na Tathmini, RTI, Mshirika mtekelezaji wa USAID inayotekeleza Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, John Noronha, amesema kuwa maeneo ya baoanuai  pamoja na yela ya hifadhi ni nyenzo muhimu kwani yamekuwa na mchango mkubwa katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.

“Ikiwa maeneo haya yataangaliwa na kutunzwa vema kwani yamekuwa yakichukua karibu asilimia 37 ya hewa chafu inayozalishwa duniani, hivyo kuendelea kufanya dunia kuwa mahala salama pa kuishi. Hata hivyo bado kuna changamoto ukiangalia mfano Dar es Salaam sehemu nyingine ya miti imekatwa lakini bado kama wanahabari hamripoti vitendo hivi kama njia salama ya kulinda mazingira yetu.

“Kadri miundombinu inavyoongezeka ndivyo miti inavyozidi kuisha bila kuja na mbinu mbadala jambo utaona kwamba linaathiri uhifadhi kwa ujumla.  Ni lazima jamii itambue kwamba baonuai ni nguzo inayofanya sayari yetu kuwa mahali pazuri kwa kuishi. Baoanuai hutoa mchango mkubwa katika maisha ya binadamu, hutupa hewa safi na maji safi, hutupa lishe bora, hutupa uelewa wa kisayansi na dawa.

“Kwa mfano hatua hii imeweza kusaidia jamii hasa katika maeneo ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara kupanda miti kwa kasi lakini kule Katavi katika kipo kijiji leo kimepata zaidi yad dola laki saba kutokana na kuuza hewa ukaa. Hatua hii ikiwa jamii itaelishwa vizuri ni wazi tunaweza kuona mchango wa baonuai hasa kwenye kutengeza kaboni kunavyochangia pato la Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa sehemu ya Utangazaji Utalii Ikolojia kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Anna Lauwo amesema kuwa  athari wa mabadiliko ya tabianchi zimenza kuonekana tangu mwaka 1976 huku kwa Tanzania ikianza mwaka 2009.

“Kwa upande wa Tanzania mwaka 2009 ndiyo ilijua kuwa tunaweza kupata madhara ya mabadiliko ya Tabianchi na mradi wa kwanza ulikuwa Babati mkoani Manyara ambao ulikuwa ukihifadhi miti na kulima matunda maji, yaani mvua ikinyesha maji yanaingia chini kisha yanahifadhiwa na miradi mingine yote hiyo ikiwa ni katika kukabiliana na mabadiliko hayo.

“Kwa hiyo hizo shughuli zimeendelea hivyo huku Serikali ikiendelea kutoa taarifa mbalimbali kwa wananchi kuhusu changamoto hii, mwaka 2014 baada ya Mkutano wa Ujerumani ikaamuliwa kwamba ili dunia iweze kurejesha uonto wake wa asili hekta milioni 350 wakakubalina kugawana kila bara ambapo Afrika ilikubali kurejesha hekta milioni 100.

“Baadae Afrika ikakaa katika kikao kilichofanyika Afrika Kusini mwaka 2014 ambapo kila nchi ilitakiwa kueleza itachangia kiwango gani kulingana na uchafuzi, ambapo TFS ilichaguliwa kuwa mratibu na ikaonekana kwamba uharibifu wa mazingira kwa Tanzania ilikuwa ni 400,960.

“… ambapo Tanzania ilisema inachangia hekta bilioni 5.2 ambapo hii inagusa maeneo na sekta mbalimbali katika kuhakikisha dunia inakuwa salama kwakuzuia athari za mabadiliko,” amesema Lauwo

Washiriki wa mjadala huo wakiwasilisha watoa mada, ambao hawapo pichani

Kutokana na hali Lauwo, amesema kuwa Serikali haiwezi kukwepa eneo hilo na imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuelimisha jamii namna bora ya kudhibiti athari za mazingira ikiwamo kupanda misitu kama inavyohimiza TFS.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here