Home KITAIFA Membe kuzikwa Mei 16, kijiji kwao Lindi

Membe kuzikwa Mei 16, kijiji kwao Lindi

Google search engine

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MWILI wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe utasafirishwa kuelekea mkoani Lindi na kuzikwa Mei 16, 2023.

Ratiba ya inaonesha Jumapili Mei 14, 2023 saa 3:30 asubuhi mwili utaagwa katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam kisha kurudishwa nyumbani kwake Mikocheni.

Mei 15, 2023 mwili utasafirishwa kwenda kijijini kwao Rondo Chiponda mkoani Lindi na Mei 16, 2023 atazikwa.

Ratiba hiyo pia inaonyesha kuwa mara baada ya mwili wa marehumu kuwasili kijijini kwao utakabidhiwa kwa wazee kwa ajili ya masuala ya mila na taratibu zingine kabla ya kukabidhiwa kwa kanisa kwa ajili ya huduma za kiroho kupitia dini yake ya Kikristo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here