Home KITAIFA Mradi Wa Maji Same – Mwanga – Korogwe kukamilika 2024

Mradi Wa Maji Same – Mwanga – Korogwe kukamilika 2024

Google search engine

Na Immaculate Makilika – MAELEZO

Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kiarabu (BADEA), Mfuko wa Maendeleo wa Nchi Zinazozalisha Mafuta (OFID) na Kuwait Fund inaendelea kutekeleza mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe ambao umelenga kusambaza maji katika Miji ya Same na Mwanga pamoja na vijiji 38 kwenye Wilaya za Same na Mwanga na vijiji vitano katika Wilaya ya Korogwe.

Hayo yamesemwa jana bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Maji kwa Mwaka 2023/24.

“Hadi mwezi Aprili 2023, kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa mtambo wa kuzalisha maji, choteo la maji, ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilomita 81.7, ujenzi wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji na ujenzi wa matanki ya kuhifadhi maji”, alieleza Mhe. Aweso.

Aidha, Mhe. Waziri Aweso alisisitiza “Ulazaji wa mabomba ya mtandao wa kusambaza maji umbali wa kilomita 105 katika Mji wa Mwanga umefikia asilimia 97 na ujenzi wa mtandao wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 102 katika Mji wa Same umefikia asilimia 99.2.

 Vilevile, kwa upande wa kipande kutoka kwenye chanzo hadi Kisangara kilichokuwa na changamoto ya mkandarasi, majadiliano baina ya Wizara na mkandarasi yamefanyika na kufikia muafaka wa mkandarasi kurejea eneo la mradi kukamilisha kazi zilizobaki”.

Waziri huyo alifafanua kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya pande zote kusaini mkataba wa makubaliano Machi 13, 2023 na utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kukamilika Mei, 2024.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here