Home KITAIFA Katibu Amcos ajinyonga kwa madai ya upotevu wa Sh milioni 118

Katibu Amcos ajinyonga kwa madai ya upotevu wa Sh milioni 118

Google search engine

Marehemu Meshaki Mwambogolo enzi za uhai wake akizungumza katika moja ya mikutano ya kichama

Na Mwandishi Wetu

-BEST MEDIA, SOMGWE

Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Ushirika AMCOS ya Shimondo iliyopo Kata ya Mlowo, Mbozi mkoani Songwe, Meshack Mwambogolo amejinyonga kutokana na madai ya upotevu wa zaidi ya Sh118 milioni ambazo ziliingizwa kwenye akaunti ya rafiki yake kisha rafiki huyo kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, ACP Theopista Mallya amesema tukio la kujingonga kiongozi huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe, limetokea jana Aprili 23, 2023 saa 11 jioni ambapo imeelezwa kwamba Mwambogolo kabla hajakutwa na mauti, alikwenda Kijiji cha Shaji ilipo ofisi ya AMCOS na kumkuta mlinzi kisha kumuomba kalamu aliyoitumia kuandika ujumbe aliouacha ndani ya gari yake.

“Baada ya kupata kalamu alitoweka akiwa na mfuko ambao ulikuwa na kamba pamoja na chupa ya sumu ya kuulia wadudu kwenye kahawa aina ya Suraban 480EC,” amesema Mallya.

Amesema kupitia ujumbe ulioachwa na marehemu kwenye gari yake anaeleza kuwa chanzo cha kujinyonga ni baada ya rafiki yake (jina tunalo) mkazi wa Mbinga kutoweka na fedha kiasi cha Sh118 milioni zilizowekwa kwenye akaunti yake ya Benki ya CRDB ili aongozane na mdogo wa marehemu aitwaye David Mwambogolo kwenda kuchukua mzigo wa kahawa Mbinga.

“Kufuatia kupotea kwa mteja huyo, mdogo wa marehemu alilazimika kumpa taarifa kaka yake kuwa hajaenda Mbinga na kuwa ametelekezwa Mbeya,” amesema Kamanda huyo.

Aidha kamanda huyo amesema uchunguzi wa tukio la kujinyonga bado unaendelea kwani inadaiwa rafiki yake huyo aliipatia AMCOS ya Shimondo tani 13 za kahawa ya maganda, na kuwa makubaliano yalikuwa apeleke kahawa nyingine na kuwa baada ya kahawa hiyo kuuza angelipwa fedha zake.

Amepongeza kuwa baada ya kumhoji rafiki yake huyo amekiri kupokea kiasi hicho cha fedha na kwamba hajatoroka na kuwa bado anaidai Shimondo AMCOS kiasi kingine cha fedha.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika AMCOS, Shimondo Mashaka Mwantepele walipoulizwa na Polisi wamekiri kudaiwa na rafiki yake huyo na kuwa bado AMCOS hiyo hajamaliza kuuza kahawa yake.

Amekutwa amefariki kwa amejinyonga usiku wa kuamikia leo kwa wazazi wake Kijiji cha Masoko kilichopo Kata ya Mlangali kwa wazazi mujibu wa mashuhuda wa tukio.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here