Home KITAIFA Mamlaka ya Anga yajivunia ubora Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius...

Mamlaka ya Anga yajivunia ubora Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere

Google search engine

NA MWANDISHI WETU, MTWARA

MKURUNGEZI Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari amesema sababu za kutua ndege kubwa duniani ya shirika la Emirates kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ni kutokana na uwanja huwa kuwa na huduma nzuri ikiwemo mipango mizuri ya dharura.

Johari ameyasema hayo leo Aprili 17, 2023 mkoani hapa, wakati akikabidhi vifaa vya ofisi kwa jeshi la polisi kituo cha Uwanja wa Ndege wa Mtwara.

Amesema ndege hiyo ilikuwa na safari ya kutoka Brazil kwenda Dubai, ilihitaji kutua na kutia mafuta, ambapo aliona kituo mbadala anaweza kwenda ni Tanzania.

“Ilitua kwa dharura kwa sababu alikuwa na safari ya kutoka Brazil kwenda Dubai na route yake lazima anapokuja lazima apite juu ya anga la Sudan , sasa Sudan sasa hivi hapajatulia kwa hiyo anga la Sudan lilikuwa limefungwa wakati yeye (rubani wa ndege ya Emirates) akiwa anakuja njiani anahitaji kutua na kutia mafuta, akaona kituo mbadala ambacho anaweza kwenda, aende Tanzania hata kama ni mbali, ” amesema.

Johari amesema ndege hiyo ilisafiri kuja mashariki na kufika Afrika Mashariki, rubani wa ndege akachagua kutua Dar es Salaam.

Johari amesema hiyo sio mara ya kwanza kwa ndege ya shirika la Emirates kutua JNIA kwa dharura, ambapo amesema mwaka 2018 ndege yenye ukubwa huo ikiwa inakwenda Mauritius na walipofika walishindwa kutua baada kukutana na hali ya hewa mbaya na wakaamua kutafuta kiwanja mbadala, ambapo walikuja kutua JNIA.

“Kwa hiyo cha kushangaza ni kwamba alitoka Mauritius alipita nchi zote angeweza kwenda Maputo, Nairobi lakini alikuja hadi Dar es Salaam ikalala, abiria wakashushwa na kupelekwa hotelini,” amesema.

Akielezea zaidi kuhusu ubora wa anga la Tanzania, Johari amesema ndege zote ambazo zinaruka katika anga hilo zinapata huduma nzuri na stahiki na kwamba anga ni salama.

“Tuna mitambo ya kisasa ya kuhudumia anga, mitambo ya kuangazia, mitambo ya sauti na mitambo ambayo inafungwa ardhini, yote tuko vizuri,” amesema.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here