Home KITAIFA Mbunge Lugangira ataja mambo manne yaliyopaisha Rais Samia miaka maiwili ya utawala...

Mbunge Lugangira ataja mambo manne yaliyopaisha Rais Samia miaka maiwili ya utawala wake

Google search engine
Mbunge wa Viti Maalumu Neema Lugangira

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

MBUNGE wa Viti Maalum, Neema Lugangira (CCM), ameyataja mambo manne aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili akiwa madarakani.

Mambo hayo ni kusimamia misingi ya haki za binadamu, utawala bora, demokrasia pamoja na diplomasia ya uchumi.

Akizungumza leo Jumanne, Aprili 4,2023 bungeni wakati akichangia mjadala  wa azimio la kumpongeza Rais Samia,Mbunge huyo amesema  katika eneo la haki za binadamu anampongeza Rais Samia kwa kuruhusu mikutano ya hadhara kufungulia vyombo  vya habari vilivyokuwa vimefungwa pamoja na kukubali kufanya maboresho ya sheria  za vyombo vya habari.

Mbunge huyo amesema anampongeza Rais  kwa kuendelea kuimarisha demokrasia ambapo alianza  hivyo kwa kuunda kikosi kazi ambacho kimemshauri katika eneo la demokrasia ya vyama vingi.

“Nikirejea katika hotuba yake aliyoitoa wiki iliyopita  katika mkutano wa Summut for democracy Mheshimiwa Rais ameahidi kwamba sheria ya vyama vya siasa inaenda kuboreshwa, sheria ya Taifa  ya uchaguzi inaenda kuboreshwa na mchakato wa katiba mpya unaenda  kuanzishwa,” amesema mbunge huyo.

Mbunge huyo amesema katika kipindi cha miaka miwili Rais Samia amefungua nchi kupitia ziara zake za nje ya nchi kwani imeweza kupatikana miradi  yenye thamani ya Sh bilioni 793.

Amesema hiyo inaonesha namna gani kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kufanya ziara nje ya nchi na  anaona fahari kusema anatoka Tanzania pindi anapokuwa nje ya nchi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here