Home KITAIFA Rais Samia amuondoa Balozi Polepole Malawi, ampeleka nchini Cuba

Rais Samia amuondoa Balozi Polepole Malawi, ampeleka nchini Cuba

Google search engine
Balozi Polepole

Na MWANDISHI WETU

RAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabdiliko ya mabalozi ya vituo vya kazi kwa mabalozi wawili na uteuzi wa Balozi mmoja.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imeeleza kuwa Rais Samia, ameBalozi Humphrey Polepole kuiwakilisha Tanzania nchini Cuba, ambapo kabla ya uteuzi huo Polepole alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

“Amemteua Balozi Luteni Jenerali Mstaafu Ycoub Mohamed kuiwakilisha Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE), kabla ya uteuzi huo Balozi Mohamed alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki,” imeeleza taarifa hiyo ya Ikulu

Pia Mkuu huyu wa nchi, amemteua Idd Seif Bakari kuwa Balozi na kumpangia Ubalozi nchini Uturuki, ambapo kabla ya uteuzi huo, Balozi Bakari alikuwa Kanseli Mkuu nchini Dubai.

Taarifa hiyo ya Ikulu imeeleza kuwa tarehe ya uapisho wa Balozi Bakari itatangazwa baadae

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here