Home KIMATAIFA Maandamano nchini Kenya : Viongozi wa Kenya wapongezwa kwa kukubali mazungumzo

Maandamano nchini Kenya : Viongozi wa Kenya wapongezwa kwa kukubali mazungumzo

Google search engine

Muungano wa Afrika Mashariki, Igad, umempongeza Rais wa Kenya William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kukubali kufanya mazungumzo yenye lengo la kumaliza wiki mbili za maandamano kuhusu gharama ya maisha na mageuzi katika mfumo wa uchaguzi.

Mnamo Jumapili, Odinga alisema kuwa muungano wake wa Azimio la Umoja-One Kenya umesitisha maandamano yake yaliyopangwa kufanyika Jumatatu kujibu kile alichokiita kuwa hatua ya rais Ruto kuonesha nia ya kufanya mazungumzo.

Katika chapisho la Twitter, Katibu mtendaji wa Igad Workneh Gebeyehu alisema hatua ya viongozi hao wawili itasaidia “kusuluhisha tofauti katika masuala ya kitaifa kwa njia za amani na kuhifadhi umoja na utaratibu wa kikatiba wa Kenya”.

Maandamano ya upinzani yaliyofutwa yangekuwa ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa maandamano yaliyofanyika Jumatatu na Alhamisi.

Unaweza pia kusoma

Kwa nini Ruto na Odinga wanakaa mezani?

Maandamano duniani: Kunani mbona kila pembe ya dunia maandamano?

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here