Home KITAIFA UCHAMBUZI ‘Tutamwambia mama’ asiwachekee manyang’au wanaofisidi nchi

‘Tutamwambia mama’ asiwachekee manyang’au wanaofisidi nchi

Google search engine
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

‘Tutamwambia mama’

Asiwachekee manyang’au wanaofisidi nchi

Na MWANDISHI WETU

Msomaji wangu wa Makala hii kwa furaha kubwa na unyenyekevu, leo ninaomba kuitambulisha kolamu hii ambayo itajukakana kwa jina la ‘Tutamwambia mama’ ikiwa na lengo la kufikisha ujumbe kwa mamlaka za Serikali kuchukua hatua dhidi ya jambo linaloweza kujikeza ndani ya jamii

Hivi karibuni Taifa letu limekuwa likishuhudia mageuzi makubwa ya maendeleo ikiwamo hatua ya Rais wa Awamu ya Sita, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa hatua yake Madhubuti ya kuifungua nchi yetu.

Ndio ni uamuzi mzuri na Madhubuti ambao siku za hivi karibuni tulishuhudia ugeni mzito wa Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris ambaye yeye pamoja na msafara wake waliweza kuzuru nchini na kufanya mazungumzo na mkuu wan chi Rais Samia Suluhu Hassan.

Moja ya jambo ambalo lilivutia ni hatua ya Serikali ya Marekani kuahidi kuunga mkono mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini, jambo ambalo kwetu tunaendelea kuona ni mageuzi makubwa sana.

Hata hivi katika masuala yetu ya ndani ya nchi narudia tena kuikipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa hatua yake ya kutoka hadharani na kupongeza taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na ile ya Takukuru ambazo zilijikita katika kuangazia upotevu na kunusuriwa kwa rasilimali za nchi yetu.

Pamoja na hatua hiyo bado Watanzania wana hamu ya kuona hatua zaidi kwa wahusika wote waliohusika na ubadhirifu huo wa fedha za umma kwa kuhakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani.

Ndio nakuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia lakini bado Watanzania wana hamu ya kuona sasa watuliotafuta na kujitengenezea zaidi fedha za malipo ya ndege yetu ya mizigo hawapo ofisini na ikiwamo wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ni wazi hatua hii itaweka wazi taswira na nia njema ya mageuzi ndani ya Serikali yao kwa kuwa na hatua Madhubuti za kudhibiti fedha za umma.

Ni kweli katika kipindi cha miaka sita iliyopita hakuna chombo cha habari wala kiongozi aliyedhubutu kutoa kauli aua hata kushauri kwa hofu kwamba mtu anaweza kupotea jambo ambalo sasa Rais Samia amefungua minyororo hiyo na si tunapaza suati kulinda rasilimali zetu.

Acha nimwambie mama pamoja na hilo bado zinatakiwa hatua zichukuliwa kwenye halmashauri zetu kwani jicho la CAG kwenye mikopo ni sehemu ndogo sana ila bado kuna fedha za miradi zimekuwa zikihujumiwa na watendaji wetu wenye maamuzi eti  hushtuka pindi madiwani wanapokuwa wanachangia hoja kwenye mabaraza.

Leo hata fedha za madarasa ya UVIKO-19  ulizopeleka kwenye kila halmashauri nchini kwetu ukiingia kwa undani bado kuna uzembe mkubwa umefanywa na watendaji wa halmashauri na hata kujiona wengine wanakumudu na kutamba wako tayari kwa lolote.

Hakika hili tunapaswa Watanzania kuungana kupinga wizi huu wa rasimali za nchi ikiwamo fedha ambazo zimekuwa zikiwanufaisha wachache kwa manufaa yao na kusahau mahitaji ya Watanzania walio wengi.

Hakika katika hili acha ‘tumwambie mama’ kwani tuna Imani naye na hana masihara katika uisimamia nchi yetu kwenye kulinda maadili na rasilimali zetu walipa kodi wa chini.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here