Home KITAIFA Ziara ya Kamala Harris imeacha matumaini kwa Tanzania, Rais Samia azidi kufungua...

Ziara ya Kamala Harris imeacha matumaini kwa Tanzania, Rais Samia azidi kufungua nchi

Google search engine

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris ameondoka nchini baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kwanza barani Afrika.

Makamu huyo wa Rais, aliwasili Tanzania Machi 29 akitokea Ghana ambako ndiko alianza safari yake ya siku tisa katika nchi za Afrika.

Anaelekea Zambia ambako atahitimisha ziara yake.

Akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Harrus amesindikizwa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango.

Katika ziara yake ya siku tatu nchini Tanzania akiwa katika Ikulu ya Magogoni jijini hapa na Mwenyeji wake Rais Dk Samia Suluhu Hassan , Makamu huyo wa Rais amempongeza Rais kwa kurejesha  Demokrasia na utawala wa sheria na wanawake kupewa vipaumbele kwenye suala la uchumi .

Aidha amesisitiza kuendelea kuboresha ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia baina ya Tanzania na Marekani.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here