Home KITAIFA Kamala Harris atembelea Makumbusho ya Taifa, awakumbuka waliopoteza maisha mabomu Ubalozi wa...

Kamala Harris atembelea Makumbusho ya Taifa, awakumbuka waliopoteza maisha mabomu Ubalozi wa Marekani mwaka 1998

Google search engine

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM


MAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Haris ametembelea Makumbusho ya Taifa leo Alhamisi Machi 30, 2023 na kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya mabomu yaliyolipuka kwenye balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998.

Kamala ametembelea mnara huo wa kumbukumbu ambao upo katika Makumbusho ya Taifa ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu nchini Tanzania.

Kabla ya kuwasili kwake, ulinzi uliimarishwa kwenye eneo hilo kukiwa na watu wachache walioshuhudia tukio hilo wakiwemo maofisa wa ubalozi wa Marekani.

Saa 9: 34 alasiri Kamala aliwasili katika viwanja vya Makumbusho na kupokelewa na waliokuwa na wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani wakati mlipuko unatokea wakiongozwa na aliyekuwa balozi Charles Stith.

Baada ya kusalimiana na wafanyakazi hao wa zamani wa ubalozi moja kwa moja Kamala alielekea eneo ulipo mnara na kuweka shada la maua kisha kuwaombea kwa dakika moja kabla ya kuondoka.

Kamala ambaye aliwasili nchini jana saa 5:20 usiku wa Machi 29, 2013, leo Machi 30, 2023 ameanza kwa mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here