Home KITAIFA ASKARI WA UHIFADHI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

ASKARI WA UHIFADHI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

&body=https://www.bestmedia.co.tz/index.php/2023/02/13/askari-wa-uhifadhi-watakiwa-kuzingatia-sheria/" title="Email" >
Email
Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-KAHAMA

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amewataka Askari wa Uhifadhi katika maeneo mbalimbali nchini wazingatie sheria kanuni,taratibu na miongozo pindi wanapotekeleza majukumu  yao ikiwemo kulinda Maliasili.

Ameyasema hayo leo Wilayani Ushetu mkoani Shinyanga mara baada ya kutembelea Kata ya Mlowa wakati wa ziara yake kikazi yenye lengo la kutatua changamoto baina ya wananchi na wahifadhi. 

 Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan inataka wananchi wake waishi kwa amani bila taharuki ya aina yoyote, hivyo Askari wa Uhifadhi wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya sheria.

“Sisi tumepewa dhamana ya kusimamia maliasili kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo, katika kutekeleza jukumu hili hatupaswi kuleta taharuki kwa wananchi,” amesisitiza Masanja.

Amewaeleza wananchi hao kuwa mtu yeyote anapovunja sheria kwa kuingia katika maeneo yaliyohifadhiwa bila vibali lazima utaratibu wa kisheria ufuatwe ikiwemo kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Aidha, ametoa rai kwa wananchi hao waendelee kufuata sheria na kuacha kuvamia maeneo yaliyohifadhiwa kwa kuwa maeneo hayo ni muhimu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Pia, amewataka Askari Uhifadhi waandae programu za kutoa elimu kwa wananchi ili wajue umuhimu na faida za uhifadhi ikiwemo kuleta mvua, kutunza vyanzo vya maji,kuchavusha mazao na kusaidia katika masuala ya ulinzi na usalama wa nchi.

Naye,Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Mboni Mhita amesema ataendelea  kushirikiana na wahifadhi kuhakikisha  elimu ya uhifadhi inaendela kutolewa kwa wananchi wanaozunguka Pori hilo.

Wananchi wakifuatilia mkutano wa Naibu Waziri Mary Masanja
Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Mboni Mhita, akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mlowa wilayani hapa
Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, Emmanuel Peter Cherehani (CCM), akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja,
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here