Home KIMATAIFA MTOTO MCHANGA NA MAMA WAOKOLEWA BAADA YA SIKU NNE CHINI YA VIFUSI

MTOTO MCHANGA NA MAMA WAOKOLEWA BAADA YA SIKU NNE CHINI YA VIFUSI

Google search engine
Picha na mtandao wa BBC

MTOTO mchanga na mama yake wameokolewa kutoka kwenye vifusi nchini Uturuki, karibu saa 90 baada ya tetemeko la ardhi la kwanza la Jumatatu.

Mtoto huyo wa kiume wa siku 10, anayeitwa Yagiz, alitolewa kutoka kwa jengo lililoharibiwa katika jimbo la kusini la Hatay.

Picha zilionyesha mtoto huyo akitolewa nje kwa uangalifu usiku kucha – tukio lililoelezwa na vyombo vya habari vya ndani kuwa la ajabu.

Matumaini ya kupata manusura zaidi yanaendelea kupungua, huku kukiwa na hali ya hewa ya baridi kali siku nne baada ya janga hilo kutokea.

Hata hivyo, juhudi za utafutaji na uokoaji zinaendelea katika Uturuki na nchi jirani ya Syria – ambayo ilikumbwa na matetemeko hayo pia.

Yagiz aliyezaliwa hivi karibuni alipigwa picha akiwa amefunikwa blanketi na kupelekwa hadi kwenye gari la wagonjwa kupokea matibabu.

Mama yake alitolewa nje kwa machela. Maelezo kuhusu hali ya afya ya wawili hao haijatolewa.

Meya wa Istanbul Ekrem Imamoglu – ambaye maofisa wake waliripotiwa kuhusika katika uokoaji – alitweet kuhusu uokoaji huo, akisema ulifanyika katika mji wa Samandag.

Picha zilizopatikana na shirika la habari la Reuters pia zilionyesha mtu akitolewa kutoka kwenye vifusi, ijapokuwa haikujulikana kama alikuwa na uhusiano wowote na wale wawili wa awali. Awali siku ya Jumatatu asubuhi la kipimo cha 7.8 na mamia ya mitetemeko mengine midogo iliyofuata.

Pia kumekuwa na hofu ya kutokea janga la pili, kwani watu wengi hawana, maji, mafuta na umeme.

Rais wa Uturuki Recap Tayyip Erdogan ameeleza kuwa ni “janga la karne”.

Wapinzani wamemtuhumu Rais Erdogan kwa kushindwa kujiandaa kwa tetemeko la ardhi na wamehoji ni vipi makadirio ya lira 88bn ($4.6bn; £3.8bn) zilizokusanywa kutokana na “kodi ya tetemeko la ardhi” zilitumika.

Ushuru huo, uliowekwa kwa mara ya kwanza kufuatia tetemeko kubwa la ardhi mwaka 1999 ambalo lilisababisha vifo vya watu 17,000 – lilikusudiwa kutumika katika kuzuia maafa na kuendeleza huduma za dharura.

Siku ya Jumatano kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki Kemal Kilicdaroglu alisema kwamba serikali ya Bw Erdogan “haijajiandaa kwa tetemeko la ardhi kwa miaka 20”.

Licha ya uharibifu huo, hadithi za watu kutoroka au uokoaji wa kishujaa zimekuwa zikiibuka katika siku zilizopita.

Maelfu ya watu wamejitolea kuasili mtoto wa kike ambaye alizaliwa chini ya jengo lililoporomoka kaskazini-magharibi mwa Syria.

Alipookolewa, mtoto Aya – akimaanisha muujiza kwa Kiarabu – alikuwa bado ameunganishwa na kitovu chake kwa mama yake, ambaye alikufa pamoja na wanafamilia wengine.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here