Home KITAIFA TANZANIA, EU KUSHIRIKIANA KWENYE UTEKELEZAJI MIRADI, KUIMARISHA UHUSIANO WA KIBIASHARA

TANZANIA, EU KUSHIRIKIANA KWENYE UTEKELEZAJI MIRADI, KUIMARISHA UHUSIANO WA KIBIASHARA

Google search engine

WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Nchi za Umoja wa Ulaya (EU).

Dk. Kijaji ameyasema hayo Februari 8, 2023 alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Mhe. Manfredo Fanti katika Ofisi za Wizara, Dodoma.

Aidha, Dk. Kijaji amemshukuru Balozi Fanti kwa ushirikiano endelevu uliopo baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuendelea kuimarika kwa Biashara kati ya Tanzania na Nchi za Umoja wa Ulaya.

Kutokana na hali hiyo Waziri, Dk. Kijaji amemueleza Balozi Fanti kuwa maandalizi ya Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Nchi za Umoja wa Ulaya yanaendelea vizuri ambapo Kongamano hilo linaloandaliwa na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya na Sekta binafsi na linatarajiwa kufanyika Februari 23-24, 2023 jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa kupitia Kongamano hilo Hati za Makubaliano mbalimbali ya Uwekezaji baina ya Tanzania na nchi za Umoja wa Ulaya zitatia saini na kutakuwa na mikutano (Session) itakayohusisha Serikali na Wafanyabiashara ambapo Viongozi mbalimbali wa Serikali wanatarajiwa kuhudhuria Kongamano hilo.

Naye Balozi Manfredo Fanti amesema kuwa ujumbe wa watu zaidi ya 600 kutoka Nchi za Umoja wa Ulaya wanatarajia kushiriki Kongamano hilo la Uwekezaji baina ya Tanzania na nchi za Umoja wa Ulaya.

Aidha, Balozi Fanti amesema kwa kuwa Tanzania inatekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini, smbspo mpango huo utachapishwa katika Tovuti ya Umoja wa Ulaya na Kongamano la Uwekezaji litakalofanyika Februari 23 hadi 24, 2023 litawaunganisha wafanyabiashara wa Nchi za Umoja wa Ulaya na Tanzania na kuchangia kuongezeka kwa uwekezaji baina ya nchi hizo

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here