Home KITAIFA Idadi ya watu China imepungua kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1961

Idadi ya watu China imepungua kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1961

Google search engine

Beijing, CHINA

Idadi ya watu nchini China imepungua kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60, huku kiwango cha uzazi nchini humo kikifikia rekodi ya chini – watoto 6.77 kwa kila wanawake 1,000.

Idadi ya watu mnamo mwaka 2022 ilikuwa bilioni 1.4118 na imepungua kwa 850,000 kutoka mwaka 2021.

Kiwango cha watoto wanaozaliwa nchini China kimekuwa kikipungua kwa miaka, na hivyo kusababisha sera nyingi kupunguza muelekeo huo.

Lakini miaka saba baada ya kutupilia mbali sera ya mtoto mmoja, imeingia kile afisa mmoja alichoeleza kuwa “zama za ongezeko hasi la idadi ya watu”.

Kiwango cha watoto kuzaliwa mnamo mwaka 2022 pia kilipungua kutoka 7.52 mnamo 2021, kwa mujibu wa Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya China, ambayo ilitoa takwimu hizo Jumanne.

Vifo pia vilizidi idadi ya waliozaliwa kwa mara ya kwanza mwaka jana – China iliingia katika kiwango cha juu zaidi cha vifo tangu mwaka 1976 – vifo 7.37 kwa kila watu 1,000, kutoka 7.18 mwaka uliopita.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here