Home KIMATAIFA Mwili wa Papa Benedict waendelea kuagwa

Mwili wa Papa Benedict waendelea kuagwa

Google search engine

Vatican, Italia

Kwa mujibu wa taarifa zilizowekwa Deutsche Welle (DW) na Vatican News, mwili wa kiongozi huyo umehifadhiwa katika Monasteri ya mama wa kanisa, ukiwa na mavazi ya kanisa badala ya jeneza kama ilivyozoeleka.

Kiongozi huyo aliyekuwa raia wa Ujerumani, alifariki Jumamosi akiwa na umri wa miaka 95, aliliongoza Kanisa Katoliki kwa muda wa miaka minane kabla ya kuwa Papa wa kwanza katika kipindi cha karne sita kujiuzulu mwaka 2013.

Mrithi wake Papa Francis ataongoza ibada ya mazishi Alhamisi katika uwanja mkuu wa Mtakatifu Peter, kabla ya kuzikwa kwenye makaburi yaliyoko katika Kanisa la Mtakatifu Petro.

Benedict alifariki katika nyumba ya watawa ya Mater Ecclesiae ndani ya bustani ya Vatican, ambayo yalikuwa makazi yake kwa muongo mmoja uliopita.

Kiongozi huyo ambaye jina lake halisi ni Joseph Aloisius Ratzinger, alipendwa na wengi, lakini alikosolewa na wengine, alikuwa Mjerumani wa kwanza kuwa Papa baada ya miaka 500 iliyopita.

Hatua yake ya kujiuzulu Februari 28, 2013 ilikuwa ya kihistoria akiwa kiongozi aliyesisitiza umuhimu wa hitaji la kiroho na wa kanisa katika ulimwengu wa kisasa ulioelimika.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here