Na Mwandishi Wetu, Best Media
KIPA namba moja wa Yanga, Djigui Diarra, amemaliza utata kwa kukubali kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na sasa atasalia Jangwani hadi 2025.
Diarra ambaye amekuwa na wakati mzuri kikosini hapo, mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika mwisho wa msimu huu.
Raia huyo wa nchini Mali, alibakiza miezi sita baada ya kusaini miaka miwili Yanga msimu uliopita na inaelezwa amekubali kuongeza miaka miwili kusalia kikosini baada ya kufanya kikao na bilionea Ghalib Said ‘GSM’ ikiwemo kuboreshewa mshahara na marupurupu mengine.