
Na KHADIJA KHAMIS
-MAELEZO, ZANZIBAR
HALI ya Mfumko wa bei ya bidhaa mbalimbali zimeongezeka kwa kipindi cha miezi 12 hadi kufikia mwezi wa septemba 2023 na kufikia asilimia 7.45 kutoka asilimia 6.82.
Akiwasilisha takwimu hizo Mtakwimu kutoka Kitengo cha Takwimu za Bei, Salma Saleh Ali amesema ongezeko hilo limechangiwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa katika kundi la chakula na vinywaji visivyo na vileo kwa kwa asilimia 13.94.
Akieleezea baadhi ya bidhaa zilizopelekea kuongezeka kwa Mfumko wa bei kwa mwaka huu amesema ni pamoja na mchele wa Mapembe kwa asilimia 37.58, Mbeya asilimia 15.13, Unga wa Ngano asilimia 3.88, Unga wa Sembe 11.02, Sukari nyekundu 29.87 nyeupe 27.3,
Akifafafanua zaidi amesema kuwa Mfumko wa bei za bidhaa za chakula wa mwaka unaoishia mwezi wa Septemba mwaka huu umeongezeka na kufikia asilimia 14.39 ikilinganishwa na asilimia 12.04 iliyorikodiwa katika mwezi wa Agosti 2023.
Hata hivyo amesema kuwa mfumko wa bei ya bidhaa zisizo za chakula kwa mwaka umepungua na kufikia asilimia 2.69 kwa mwezi wa Septemba 2023 ikilinganishwa na asilimia 3.22 iliyorikodiwa katika mwezi wa agosti 2023.
Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, Ultrick amesema kuwa ongezeko la bei ya bidhaa za chakula na sisizo za chakula zimetokana na kupanda kwa bei ya mafuta pamoja na uhaba wa upatikanaji wa dola.