Ndege mpya aina ya Boeing 737 Max 9 ipo angani kutokea Mji wa Seattle, Marekani kuja Tanzania. Ndege hiyo itwasili nchini Oktoba 3, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Terminal I. Mapokezi ya Ndege hiyo yataongozea na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Philip Isor Mpango.